Recent comments

Breaking News

LULU ahukumiwa kifungo cha Miaka Miwili Jela

Mahakama Kuu ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania
imemhukumu kwenda jela
miaka miwili muigizaji wa
filamu bongo Elizabeth
Michael (Lulu) ambaye
alikuwa anakabiliwa na
kesi ya kuua bila
kukusudia.
Hukumu hiyo imetolewa leo
na Jaji Sam Rumanyika
aliyekuwa anaendesha kesi
hiyo, na kusema kwamba
mshtakiwa amekutwa na
hatia ya kuua bila
kukusudia kutokana na
ushahidi wa mazingira,
hivyo atatumikia kifungo
cha miaka miwili jela.
"Ushahidi wa mazingira
unaweza kutumika kama
msingi pekee wa kumtia
hatiani mshtakiwa tena
mshtakiwa pekee, sasa
ninapokwenda kuangalia
maelezo ya mshtakiwa
kama yanakidhi vigezo
nilivyosema awali, kwa
mujibu wa mshtakiwa
alisema alianza kupigwa na
marehemu, marehemu
alilewa lakini kuhusu
mshtakiwa anatakiwa kutoa
maelezo yanayo jitosheleza,
kwa hili mshtakiwa
alijikanganya" amesema
Jaji Rumanyika.
Jaji Rumanyika ameendelea
kwa kusema
kwamba.."mshtakiwa katika
maelezo yake hakueleza
kuwa marehemu alianguka
au laah wakati
anamkimbiza, maelezo ya
Dkt. Josephine siyo
maelezo ya cheti cha
hospitali, hayakuwa na
hadhi ya hospitali".
"Inakinzana na hekima ya
kawaida kwamba hata pale
marehemu alipoendelea
kumpiga na kumshambulia
na akaenda kiwango cha
kumtishia kumuua,
mstakiwa hakuthubutu hata
kumpiga, ina maana
alifanya kama maneno ya
biblia yanavyosema mtu
akikupiga shavu la kushoto
mgeuzie na la kulia lakini
hili mshtakiwa
hakulisema.", amesema Jaji
Rumanyika.
"Na wakati huo mshtakiwa
alikuwa na miaka 17, leo
ana miaka 22, alikuwa
mtoto hivyo asingetambua
kuwa kinachofanyika ni
kibaya au kizuri, huyu
mtoto sio mshtakiwa
aliyelengwa nasheria ya
watoto, kama mtoto wa
umri huu na anaweza
kafanya ya watu wazima,
mahakama hii haikubaliani
bali mshtakiwa ni
mkomavu, hakuna mashaka
kuwa kifo cha marehemu
kilitokana na ugomvi",
ameendelea kusema Jaji
Rumanyika mahakamani
hapo.
Baada ya hapo jaji
rumanyika aliwapa nafasi
upande wa mshtakiwa
kujitetea ambapo wakili
wake Peter Kibatala
alimtetea mshakiwa kwa
kusema kuwa mshtakiwa
anategemewa na familia
yake.
Baada ya hapo Jaji
Rumanyika alitoa hukumu
yake na kumuamuru
mshtakiwa kwenda jela
kwa miaka miwili.
Elizabeth Michael (Lulu)
anahukumiwa kwa kumuaa
aliyekuwa mpenzi wake
Steven Charles Kanumba
ambaye pia ni muigizaji
mwenzake, mnamo April 7,
2012.

No comments