Recent comments

Breaking News

WADADA MNISAMEHE KIDOOOGO!..


Wanaume wengi hawajafikia ndoto zao, wanatamani kupata wanawake watakaowatia moyo kuwafikisha kwenye ndoto zao! Ukweli mchungu ni kwamba wanawake hawawataki wanaume ambao bado wako safarini kuelekea ndoto zao! Wanataka waliokwisha fika, na bahati mbaya zaidi waliokwisha fika wako 'occupied !! Linalotokea ni nini?! Wanawake wanadhani wana bahati mbaya ?!.
Unaweza kuwa unalalamika kuwa una mkosi wa kuolewa yaani kila mwanaume anakuja na ahadi nzuri, baadae anakuacha! Lakin upande mwingine huenda maamuzi yako ndiyo maumivu yako.
Kweli huenda we ni mtoto wa kike mzuri wa sura umbo na hata kila kitu ila umenyimwa hekima!
Una mpaparikia kijana mtanashati kisa ana gari na kazii nzuri. Unamwona kijana anaeenda kumbi za usiku ndo mjanja, anae vaa suruali chini ya makalio ndo sahihi kwako lakini yule anayeenda ibada kila ijumaa au jumapili unamwona mruga ruga tu!.
Una mpuuza na kumdharau mtu 'A' kisa tu yeye ni kijana aliye soma ila hana ajira. Ama ni kijana ambae kipato chake hakizidi laki 2 kwa mwezi badala yake una mkumbatia mtu 'B' ambae ni baba fulani na ni mume wa fulani kisa tu anapesa na shida zako zote anakutatulia...!!
SWALI!!
Utaolewa vipi ikiwa mpaka sasa unapenda kutoka na waume za watu au vijana wenye magari ya mikopo, au kijana yeyote ambaye unajua huna future naye? Au ndo unam'please ili asiache kukupa pesa!? Nani atakae KUOA wakati vijana wanaotafuta mke wewe una wasema vibaya kuwa hawana hadhi ya kutembea na wewe kisa hawana misuli ya uchumi kwa muda huo?..
Funguo ya NDOA utaipata wapi wakati hapo ulipo una mnunia mke wa mtu kisa una toka na mume wake?
Dada maisha yanabadilika mwanaume mpiga debe wa leo kesho unaweza mbadilisha akawa dereva kisha akamiliki gari lake...hakuna mtu aliye zaliwa kuwa masikini ndo maana juhudi zinahitajika... Mwanaume anae tumia pesa kukufanya uwe wake anafanya hivyo kwa wengi ila usijifanye hujui kisa unafaidika jua muda unaenda.
Weka malengo mbele lini unatamani uwe na ndoa yako na umri gani uzae kuliko kufanya anasa. Mwaka wa ngapi huu bado unatoka na wanaume ambao hawana malengo Na wewe, kazi ni pombe na wanawake?.
Umegombana Mara ngapi na huyo HB wako kisa usaliti na bado upo nae?? Wanaume wangapi wenye pesa mvuto na kila kitu ndani lakini wamekutumia na kukuacha? Lakini bado hujifunzi aina ya mwanaume wa kuwa nae?
Japo vyema acha kujidharau u mrembo onesha kwamba unajipenda kuanzia MAVAZI NA KAULI !
Marafiki zako wangapi waliolewa na wanaume wa kawaida lakin leo wana mafanikio? Kwa nini usiige..weka uzuri pembeni simama imara kama MKE na MAMA bora wa kesho. Mtie moyo mmeo ajisifu kuwa na wewe, si kila mara dharau na kumbeza!!
Kifupi hakuna mwanamme anayependa mke asiyemtia moyo kwa kile kidogo anachofanikiwa kufanya !! Encouragement matters most kwa mwanaume yeyote mwenye akili timamu!.
Dada yangu muandae leo Bill Getes wako leo, Said Salim Bakharesa wako leo au Muhamed Deuj "Mo" wako leo..

AHSANTE.... SHARE NA WENZAKO

No comments