Recent comments

Breaking News

Nemc yafungia kiwanda cha mifuko

Kiwanda hicho kilichopo Kijiji cha Mwanambaya, Kata ya Tambani Wilaya ya Mkuranga, pia kimepigwa faini ya Sh5 milioni baada ya kuidanganya Nemc kuwa hakijaanza utengenezaji wa mifuko wakati wakiwa tayari wameanza uzalishaji.
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc) limekifungia kiwanda cha katengeneza mifuko maarufu kama 'viroba' cha Bubugao Footwear Co Limited baada ya kuanza uzalishaji bila kibali cha tathimini mazingira.
Kiwanda hicho kilichopo Kijiji cha Mwanambaya, Kata ya Tambani Wilaya ya Mkuranga, pia kimepigwa faini ya Sh5 milioni baada ya kuidanganya Nemc kuwa hakijaanza utengenezaji wa mifuko wakati wakiwa tayari wameanza uzalishaji.
Mratibu wa Mazingira Kanda ya Mashariki, Jaffar Chimgege amesema wamefikia uamuzi huo baada ya  kufanya ukaguzi na kubaini kiwanda hicho kimeanza kazi ya utengenezaji wa mifuko hiyo hali kikiwa hakina kibali cha mazingira kutoka Nemc.
Kaimu Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Qiu Huashi amekiri kuendesha kiwanda bila kibali na kuahidi kufuata sheria ikiwamo kutekeleza maagizo aliyopewa na Nemc ili kiweze kufunguliwa.

No comments