Recent comments

Breaking News

Tuna Picha ya Diamond na Ali Kiba Wakiwa Wanaongea – Babu Tale


Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Jumanne hii, Babu Tale amewataka mashabiki wa muziki kuamiani kwamba yeye pamoja na Diamond hawana tatizo na Ali Kiba.

Mmoja kati ya viongozi wa juu wa label ya ‘WCB’, Babu Tale amesema watu hawajui kama Ali Kiba na Diamond wakikutana wanazungumza kama kawaida.
Amesema hayo baada ya weekend hii kuzagaa picha katika mitandao ya kijamii inayomuonyesha Babu Tale, Sallam, Ommy Dimpoz, Mwana FA pamoja Ali Kiba wote wakiwa na nyuso za furaha hali ambayo liibua maswali mengi kwa mashabiki.

“Unajua binadamu wanatakiwa kubadilika, huwezi ukatengeneza dhana sisi tuna matatizo hatuwezi hata kupiga picha, hatuwezi kukaa pamoja, hatujafikia hatua hiyo, sisi tunabishana kimuziki na tunatengeneza value ya muziki ili muziki wa Tanzania ukue,” alisema Tale.

Aliongeza, “Haimaanishi Diamond na Ali Kiba wakikaa hawaongei, watu hawajui kuna picha ambazo sisi tunazo Diamond na Kiba wanaongea wapo studio kabisa. Hata kama tukiamua kizipost hizo watu wangeanza kuzungumza zitu vingine, picha ni kitu cha kawaida. Katika hii picha ambayo inazungumziwa alianza kuitwa Mwana FA, akaitwa Omary, akaitwa Ali, tukaitwa mimi na Sallam, kama ningekuwa sitaki kukaa karibu na Kiba ningekimbilia moja kwa moja kwa na Sallam kwa sababu sisi ni wamwisho kuitwa,”

Diamond na Ali Kiba ni wasanii ambao wanadaiwa hawaelewani kitu ambacho kimekuwa kikikanushwa na pande zote mbili.

No comments